Mwongozo wa kuanza
Weka ShelfWise mwenyewe, hatua kwa hatua
Kuanzia bidhaa yako ya kwanza hadi msafirishaji mlangoni kwa mteja wako. Kila hatua ina kiungo chake, ili umtumie mtu hatua hasa anayoihitaji.
Weka biashara yako
Akaunti yako, mipangilio, bidhaa, timu na matawi.
- 1 Fungua akaunti yakoJisajili kwa dakika chache na uanze majaribio ya bure ya siku 14.
- 2 Angalia mipangilio ya biashara yakoJina la biashara, aina, mahali, lugha na saa za eneo.
- 3 Ongeza bidhaa zakoJina, bei, stoku na picha, moja moja au kutoka spreadsheet.
- 4 Wape timu yako akaunti zaoAlika mameneja na wafanyakazi, kila mmoja na anachohitaji tu.
- 5 Ongeza matawi yakoKila tawi lina stoku, mauzo na oda zake.
- 6 Iweke kulingana na aina ya biashara yakoMaduka, mikahawa na baa, saluni na maduka ya dawa kila moja linapata mpangilio wake.
Uza na ufuatilie mauzo yako
Till, hesabu za leo na M-Pesa inayolinganishwa na kila mauzo.
Duka la mtandaoni na usafirishaji
Kiungo cha duka lako, oda zinazolipwa kwa M-Pesa, wasafirishaji wako na ufuatiliaji wa moja kwa moja.
- 10 Fungua duka lako la mtandaoniKiungo cha duka lako chenye bidhaa zako, maeneo ya kuletewa na kulipa kwa M-Pesa.
- 11 Pokea oda zikiwa tayari zimelipwaWateja wanaagiza kwenye simu, wanalipa kwa M-Pesa na oda inakufikia.
- 12 Ongeza wasafirishaji wakoOngeza kila msafirishaji na uunganishe simu yake kwa namba ya siri.
- 13 Sakinisha programu ya ShelfWise RiderWasafirishaji wako wanapata kila oda na maelekezo, na wateja wanawafuata moja kwa moja.
- 14 Tuma oda na umfuatilie msafirishajiMpe msafirishaji oda, mfuate kwenye ramani, na mauzo yanajirekodi yenyewe.
Ungependa tukuwekee?
Tunatembelea biashara yako, tunaweka bidhaa zako, tunaunganisha M-Pesa na kuwasha duka lako la mtandaoni na wasafirishaji. KSh 3,000, mara moja.
Omba tukuwekee